Zaidi ya tiketi laki 8 zauzwa mpaka sasa Kombe la Dunia QatarMashabiki wa kandanda wamenunua tiketi 804,186 za mechi za Kombe la Dunia nchini Qatar baadae mwaka huu katika awamu ya kwanza ya uuzajii.


Shirikisho la kandanda Duniani na waandalizi wa kinyang'anyiro hicho FIFA wamesema wanunuzi wengiwa tiketi hizo wametokea Qatar, Marekani, England, Mexico, Umoja wa Falme za Kiarabu, Ujerumani, India, Brazil, Argentina na Saudi Arabia.


Tiketi za mechi ya ufunguzi mnamo Novemba 21 mwaka huu ambayo itaihusisha wenyeji Qatar pamoja na fainali ya Desemba 18 ndizo zilizonunuliwa kwa wingi.


Timu 32 zitashiriki tamasha hilo na mpaka sasa 27 tayari zimefuzu. Droo ya mwisho ya Kombe la Dunia ambapo timu zitapangwa katika makundi itafanyika Ijumaa Aprili mosi.

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu