Waziri mkuu wa zamani wa Japan auawa kwa bunduki ya kutengenezwa kwa mkono,muuaji atambulikaMtu anayeshukiwa kumpiga risasi Waziri Mkuu wa zamani wa Japan Shinzo Abe ametambuliwa na vyombo vya habari vya Japan kama Tetsuya Yamagami mwenye umri wa miaka 41, mkazi wa mji wa Nara.


Anaripotiwa kuwa mwanajeshi wa zamani wa Kikosi cha Kujilinda cha Majini cha Japan, jeshi la wanamaji la nchi hiyo, lakini wizara ya ulinzi haijathibitisha rasmi hili.


Mtangazaji wa shirika la serikali la Japan NHK aliripoti kuhusu Yamagami akiwaambia polisi kuwa ‘’hajaridhika na Abe na alitaka kumuua.’’


Mshukiwa sasa yuko chini ya ulinzi wa polisi.


Walioshuhudia walisema walimwona mtu akiwa amebeba kile walichotaja kuwa ni bunduki kubwa na kumfyatulia risasi Abe mara mbili kwa nyuma.


Picha zilizopigwa wakati mshukiwa anakamatwa zinaonyesha kile kinachoonekana kama silaha iliyoboreshwa.


Haijulikani ni vipi mpiga risasi huyo alikuja kujua kuhusu kuhudhuria kwa Abe kwenye kampeni mapema, kwani ziara hiyo ilithibitishwa jana usiku.

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu