Waziri mambo ya nje Marekani apata CoronaWaziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken amepimwa jana Jumatano na kukutwa na maambukizi ya COVID-19 na atafanya kazi kwa njia ya mtandao.

Wizara ya mambo ya nje iya Marekani imesema waziri huyo amepata chanjo kamili pamoja na Booster dhidi ya virusi hivyo.

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje Ned Price amesema kuwa Blinken hatoweza kutoa tena hotuba iliyokuwa ikisubiriwa kwa muda mrefu kuhusu sera ya China ambayo ilipangwa Alhamis hii.


Anatarajia kurejea kwenye jengo la wizara hiyo na kuanza tena ratiba yake kamili pamoja na safari haraka iwezekanavyo ilisema taarifa hiyo.

Blinken alikuwa miongoni mwa wageni waliojazana katika hoteli ya Washington siku ya Jumamosi kwa ajili ya chakula cha jioni cha kila mwaka cha chama cha waandishi wa habari wa White House.


Trevor Noah mchekeshaji ambaye alimtambulisha Rais Biden alitania kuhusu chakula hicho cha jioni kuwa ni tukio kubwa la kusambaza virusi.

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu