Watu zaidi ya mia tisa wafariki tanu kuanza kwa vita UkraineOfisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa imesema kuwa idadi ya raia waliouawa nchini Ukraine tangu kuanza kwa uvamizi wa Urusi tarehe 24 Februari imefika 925, na waliojeruhiwa ni 1,496 kufikia usiku wa kuamkia leo.


Taarifa hizo zinakuja wakati Ukraine ikiwa imekaidi matakwa ya Urusi kuwa wanajeshi wake wasalimu amri katika mji wa Mariupol, ili waweze kupatiwa njia ya kuondoka katika mji huo wa bandari uliozingirwa.


Ukraine imeitolea wito China kuwa na jukumu muhimu katika kusuluhisha mizozo, ukiwemo ule baina yake na Urusi.


Uvamizi huo wa Urusi umeingia katika wiki ya nne, bila kufanikiwa kuudhibiti kikamilifu mji wowote muhimu wa Ukraine, ukiwemo mji mkuu, Kiev.


Wakati huo huo, Urusi imepiga marufuku mitandao ya kijamii ya Facebook na Instagram nchini humo, baada ya mahakama kuikuta mitandao hiyo inayomilikwa na kampuni ya Meta, na hatia ya misimamo ya chuki.

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu