Watu 35 wauawa katika mashambulizi ya anga ya UrusiRaia 35 wameuawa na wengine zaidi ya 130 kujeruhiwa katika mashambulizi ya anga yaliyofanywa na vikosi vya Urusi. Mashambulizi hayo yalikilenga kituo cha kijeshi katika mji wa Ukraine wa Lviv karibu na mpaka na Poland. Kituo hicho kilikuwa kikitumiwa na Ukraine katika Luteka za kijeshi na nchi za jumuiya ya kujihami NATO. Marekani siku ya Jumamosi iliidhinisha nyongeza ya dola milioni 200 za vifaa vya kijeshi kwa ajili ya Ukraine. Lakini Urusi ilionya kwamba majeshi yake yangeweza kulenga shehena za silaha zinazosambazwa na nchi za magharibi. Raia wengi wa Ukraine walikuwa wamekimbilia katika mji wa Lviv tangu uvamizi ulipoanza kwa ajili ya usalama wao. Wakati huo huo rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy amesema raia wapatao 125,000 wamehamishwa kupitia njia salama ya kiutu.

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu