Watoto wachanga 11 wafariki kwa moto katika hospitali SenegalWatoto 11 waliozaliwa wamefariki kwenye moto uliotokea katika hospitali moja iliyopo mji wa Tivaouane, magharibi mwa Senegal, rais wa nchi hiyo alisema siku ya Jumatano.


Rais Macky Sall alisema "kujifunza kwa uchungu na kufadhaika kuhusu vifo vya watoto 11 wachanga katika moto uliotokea kwenye idara ya watoto wachanga ya Hospitali ya Mame Abdou Aziz Sy Dabakh huko Tivaouane".


"Kwa mama zao na familia zao, ninawapa pole sana," Sall alisema kupitia ukurasa wake wa Twitter.


Tivaouane iko karibu 120km (maili 75) mashariki mwa mji mkuu, Dakar.


Moto huo ulisababishwa na "Shoti ya umeme", mwanasiasa wa eneo hilo Diop Sy alinukuliwa akisema.

Hospitali hiyo inasemekana ilizinduliwa hivi karibuni.

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu