Watatu wauawa na wengine wengi wajeruhiwa kwenye shambulizi la bunduki

Watu watatu wameuwawa na wengine wengi kujeruhiwa jana baada ya mtu aliyejihami kwa bunduki kufyatua risasi katika eneo moja la maduka mjini Copenhagen huko Denmark.


Polisi wa Denmark wanasema wamemkamata mtu mmoja mwenye umri wa miaka 22 raia wa Denmark na wakamfungulia mashtaka ya kuuwa pasipo kukusudia.


Mshukiwa huyo amepatikana pia akiwa amebeba bunduki.


Mkanda wa video kutoka kwenye vyombo vya habari nchini humo umeonyesha makundi ya wateja wenye wasiwasi wakikimbia kutoka kwenye duka hilo. Katika taarifa, Waziri Mkuu wa Denmark Mette Fredrikesen amewataka Wadenmark kuonyesha mshikamano katika kile alichokiita "wakati mgumu kwa taifa hilo."


Shambulizi hilo linafanyika baada ya wiki ya furaha nchini humo kwani ilikuwa mwenye wa mashindano ya baiskeli ya Tour de France.

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu