Wasababisha kifo cha mtoto kwa kumnyima huduma za afyaWatu 12 waumini wa kikundi cha kidini wamekamatwa kwa kusababisha kifo cha mtoto wa miaka nane nchini Australia.


Elizabeth Struhs alifariki Januari 7 nyumbani kwao kusini mwa Brisbane, baada ya binti huyo aliyekuwa mgonjwa wa kisukari aina ya kwanza kudaiwa kunyimwa insulini kwa karibu wiki.


Mapema mwaka huu, wazazi wake walishtakiwa kwa mauaji, mateso na kushindwa kutoa mahitaji muhimu katika maisha ya mtoto huyo.


Polisi sasa wanasema watawafungulia mashtaka watu wengine 12 wenye umri wa kati ya miaka 19 na 64 kutokana na kifo cha mtoto huyo.


Kundi hilo lilikuwa linajua hali ya afya ya Elizabeth kuwa mbaya lakini hawakutafuta msaada na badala yake walimuombea Elizabeth apone alipokuwa akiugua sana, Polisi wa Queensland walisema katika taarifa.


Mamlaka haikuitwa hadi siku moja baada ya mtoto kufariki.


Kaimu Msimamizi wa Upelelezi Garry Watts alisema polisi wameshangazwa na walichokipata.


"Katika miaka yangu 40 ya upolisi, sijawahi kukumbana na jambo kama hili," alisema.


Wazazi wa mtoto huyo walikuwa sehemu ya madhehebu yenye imani "zilizoongozwa na woga na udhibiti" ambayo huchukulia dini katika viwango vya kupita kiasi.


Watu hao 12 waliokamatwa Jumanne wanatarajiwa kufikishwa mahakamani siku ya Jumatano.

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu