Wanaume washauriwa kupima tezi dume, kidole hakitumiki tenaWataalamu wa afya wamewataka wanaume kuwahi mapema kupima saratani ya tezi dume kwa kuwa kipimo kilichokuwa kikifanyika kwa njia ya kidole kwa sasa hakitumiki tena kutokana na kukua kwa teknolojia.


Na sasa kipimo kinachotumika sasa ni kile cha damu ambayo huchunguzwa protini maalum ya tezidume (PSA) na kipimo cha kuchunguza ukubwa na umbo la tezidume, hufanyika kama vipimo vya awali.


Hayo yamesemwa Machi 17 2022 na Daktari bingwa wa magonjwa ya saratani kutoka Taasisi ya Saratani Ocean Road (ORCI), Caroline Swai alipokuwa akiutambulisha mradi wa kupambana na saratani (TCCP) kwa vyombo vya habari.


Mradi huo unatekelezwa mkoani Mwanza na Dar es Salaam kwa ushirikiano kati ya Taasisi ya Afya ya Aga Khan Tanzania (AKHST) na taasisi za umma za afya.


“Sayansi inabadilika kila wakati, suala la kuwapima wanaume na kidole kwa sasa halipo na nji ahiyo haipendelewi na wanaume wengi, hii ilitumika zamani wakati hatuna vifaa, ilikuwa ukiingiza kidole kama tezi dume imevimba unaitambua kwa kugusa vimbe ambazo zinakuwa kama madungulidunguli,” amesema Dk Swai


“Maendeleo ya teknolojia na sayansi kwa sasa tunagundua mapema na inakuwa bado laini huwezi kuitambua kwa njia ya kidole hivyo tunawafanyia kupitia kipimo maalum cha damu na tunabaini hata kama kuna seli zimeanza kujikusanya, hivyo wanaume wasiogope wajitokeze kutambua hali zao mapema.”

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu