Wananchi walazimisha kuvamia makzi ya waziri mkuu Srilanka

Waziri Mkuu wa zamani wa Sri Lanka Mahinda Rajapaksa ameondoka katika makaazi yake leo baada ya jeshi kuzuia majaribio kadhaa ya waandamanaji wanaoipinga serikali kuingia kwa nguvu nyumbani kwake jana usiku.


Polisi imesema jeshi lilifyatua risasi angani na kutumia mabomu ya kutoa machozi ili kuwafurusha waandamanaji nje ya makaazi rasmi ya waziri mkuu, yanayofahamika kama Temple Trees katika mji mkuu Colombo.


Waandamanaji pia wameteketeza kwa moto zaidi ya nyumba 70 na ofisi za mawaziri wa zamani na wabunge wa chama tawala na zaidi ya magari 150 yamechomwa moto au kuharibiwa.


Rajapaksa alijiuzulu jana baada ya wafuasi wa chama tawala cha Sri Lanka Peoples Front - SLPP kupambana na waandamanaji mjini Colombo.


Waandamanaji wanamtaka Rais Gotabaya Rajapaksa, ambaye ni kakake Mahinda, pia naye ajiuzulu.

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu