Wanakamata mabinti wanawazalisha na kuuza watoto wapata fedhaTakriban vijana 35 wameokolewa kutoka katika kile kinachoitwa ‘’kiwanda cha watoto’’ nchini Nigeria.


Habari zaidi zinasema wanawake na wasichana hutekwa na huwekwa ili kuzaa watoto kwa ajili ya kuuzwa.


Mamlaka ilisema wasichana wanne katika jengo hilo katika jimbo la kusini-mashariki la Anambra walikuwa tayari wajawazito.


Msemaji wa polisi Torchukwu Ikenga aliiambia BBC kuwa washukiwa watatu wamekamatwa - wanaotuhumiwa kuwateka nyara vijana hao pamoja na kuwahusisha katika utumwa wa ngono, ukahaba na kuendesha kiwanda cha watoto.


Polisi walipata bunduki tatu wakati wa uvamizi kwenye jengo hilo katika mji wa Nkpor, karibu na mji wa kibiashara wa Onitsha.

Eneo hili kwa kawaida huendeshwa na magenge ya biashara haramu ya binadamu - baadhi katika majengo yaliyojificha kama kliniki za uzazi au hoteli.


Licha ya juhudi za mara kwa mara za mamlaka kwa miaka mingi kuzifunga - zinaendelea kufanya kazi kwa siri.

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu