Wanajeshi wa Sudan waishambulia EthiopiaWanajeshi wa Sudan wametekeleza mashambulizi dhidi ya vikosi vya Ethiopia katika eneo la mpaka unaozonaziwa la Al Fashaga kufuatia madai ya mauaji ya wanajeshi wake saba.


Ripoti za walioshuhudia zinasema kwamba walisikia milio mikubwa ya milipuko na sauti kali za risasi huku Jeshi la Sudan likitekeleza mashambulizi ya angani na ardhini.Hali ya wasiwasi kuhusu eneo hilo linalozozaniwa imeendelea kwa kipindi cha mwezi mmoja sasa.


Mapema Sudan ilitangaza imefunga mpaka wake na Ethiopia kuhusu mauaji hayo.


Khartoum pia imemrudisha nyumbani balozi wake nchini Ethiopia na kumtaka balozi wa Ethiopia nchini humo kuelezea chanzo cha mauaji hayo.


Sudan inasema kwamba wanajeshi hao ambao walikuwa wakishikiliwa mateka waliuawa na miili yao kuoneshwa kwa umma .

Ethiopia imekana madai hayo na badala yake kulishtumu jeshi la Sudan kwa kuingia katika ardhi yake.

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu