Wanajeshi Cameroon wadaiwa kuua raia 10 wasio na hatiaWanajeshi katika eneo la kaskazini magharibi la Cameroon wanatuhumiwa kuwauwa watu kadhaa wakati wa msako wao dhidi ya waasi wanaotaka kujitenga kwa eneo hilo.


Kwa mujibu wa shirika la haki za binaadamu la Human Righs Watch, kwa uchache watu 10 waliuawa baina ya mwezi Aprili na Juni mwaka huu wakati wanajeshi wa Cameroon walipolivamia eneo hilo kwa madai ya kuwasaka waasi waliojitangazia uhuru wa nchi waiitayo Ambazonia.


Watu wengine 17 wanaaminika kuwa wametoweka mikononi mwa vyombo vya dola. Ripoti hiyo iliyotolewa jana na Human Rights Watch inakuja wakati waangalizi wengine pia wakiituhumu serikali ya Cameroon kwa ukiukaji mkubwa wa haki za binaadamu kwenye mapigano yake na waasi.


Mikoa ya kusini magahribi na kaskazini magharibi mwa Cameroon inakaliwa na raia wanaotumia Kiingereza kama lugha rasmi na ambao ni asilimia 17 ya Wakameruni wote.

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu