Wanafunzi 30 wadungwa sindano moja India,uchunguzi waanzaAfisa mmoja wa Afya anacahunguzwa kwa kuwadunga sindano moja wanafunzi 30 katika jimbo la kati nchini India la Madhya Pradesh.


Tukio hilo lilifanyika katika shule moja iliopo wilaya ya Sgar ambapo Watoto waolikuwa wakipatiwa chanjo ya Corona.

Wizara ya Afya nchini India Inaruhusu kila mtu kutumia sindano yake , ikiwa ni masharti ya corona.


India imetoa chanjo bilioni 2.03 za corona kufikia sasa.


Sindano zinazotumika mara moja hutumika sana nchini India ili kuzuia kusambaa kwa magonjwa hatari kama vile HIV.


Hatahivyo kumekuwa na matukiko kadhaa siku za awali ambapo sindano moja imetumika zaidi ya mara moja kutokana na uhaba wa vifaa.


Jitendra Rai ambaye alikuwa anawapatia chanjo hiyo watoto , aliambia vyomabo vya habari kwamba alipatiwa sindano moja n idara ya afya na kwamba alikuwa akifuata maagizo.


Wazazi walioambatana na watoto wao waliona tatizo hilo na kuliripoti kwa usimamizi wa shule hiyo.

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu