Waliouawa kwa risasi klabu ya usiku wafikia 19 Afrika kusiniMatukio mawili ya ufyatuaji risasi nchini Afrika Kusini yamesababisha vifo vya watu 19.


Mauaji hayo yametokea katika kitongoji kimoja karibu na mji wa Johannesburg, na jingine mashariki mwa nchi hiyo.


Polisi wanafanya uchunguzi kama matukio hayo mawili yanahusiana.


Kwenye kitongoji cha Soweto, watu 15 waliuawa katika klabu ya usiku, wakati watu waliokuwa na silaha waliwasili kwenye basi dogo na kuwamiminia watu risasi kiholela.


Katika eneo la Pietermaritzburg katika mkoa wa KwaZulu-Natal, polisi wamesema watu wanne waliuawa na wengine wanne kujeruhiwa kwenye baa wakati wanaume wawili walianza kufyatua risasi kiholela.

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu