Waliopindua serikali nao wanusurika kupinduliwa nchini MaliSerikali ya kijeshi nchini Mali imesema imezuia jaribio la mapinduzi ya serikali, jaribio ambalo lilifadhiliwa na mataifa ya magharibi kupitia kwa wanajeshi waatiifu kwa mataifa hayo.


Kupitia taarifa uongozi wa kijeshi nchini Mali, umesema jaribio hilo la mapinduzi lilifanyikaa usiku wa tarehe 11 na 12 mwezi huu.


Bila kutoa maelezo Zaidi serikali ya Mali, imesema jaribio hilo la kupindua serikali lilikabiliwa kitaalamu na waliohusika wapatao maafisa 10 wa jeshi watakabiliwa kisheria, bila pia kutaja wahusika.


Wanajeshi wa Mali wametekeleza mapinduzi ya serikali mara mbili tangu mwaka 2020, baada ya kumuondoa madarakani rais Ibrahim Keita, utawala wa sasa ukishinikizwa kurejesha utawala wa kiraia.

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu