Wakazi wa Nagasaki Japan waadhimisha miaka 77 ya shambulio la bomu la AtomikiWakazi wa mji wa Nagasaki nchini Japan leo Agosti 9 wamefanya kumbukumbu ya miaka 77 ya shambulio la bomu la atomiki.


Katika hotuba yake kwenye uwanja wa amani wa Nagasaki, Meya wa jiji Tomihisa Taue, amesema vita vya Urusi na Ukraine vinaleta kitisho kingine cha shambulizi la nyuklia.


Aidha meya huyo amesema silaha za nyuklia zinaweza kutumika maadamu bado zipo katika uso wa dunia na kuangamizwa kwake ndio suhusho pekee la kuunusuru ulimwengu.Itakumbukwa Agosti 6, 1945, Marekani ilifnyatua kombora la kwanza la atomiki duniani katika mji wa Hiroshima kulivuruga kabisa jiji hilo na kuwauwa watu 140,000.


Siku tatu baadaye, Marekani ikaushambulia tena mji wa Nagasaki na kuwauwa watu wengine 70,000.

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu