Wakamatwa na magunia zaidi ya elfu moja yenye nyama ya PundaPolisi nchini Nigeria wamekamata magunia 1,390 ya nyama ya punda katika jimbo la kaskazini-magharibi la Kebbi karibu na mpaka na Niger.


Mkuu wa masuala ya ushuru wa forodha Joseph Attah amesema uchunguzi wa awali ulionyesha takriban punda 1,000 walichinjwa na nyama zao kuwekwa kwenye magunia kwa ajili ya kusafirishwa.


Amesema usafirishaji huo wa nyama ya Punda ni katika muendelezo wa biashara haramu ya wanyamapori inayofanywa na baadhi ya watu nchini humo.


Magunia hayo yalikuwa yakisafirishwa kwa lori ambalo halikufahamika mara moja lilikoelekea.


Dereva wa lori hilo na mshukiwa mwingine mmoja wamekamatwa na watafunguliwa mashtaka, maafisa walisema.


Nigeria imekuwa ikijitahidi kukabiliana na mauaji ya punda na biashara haramu ya sehemu zao huku idadi ya wanyama hao ikiendelea kupungua kwa kasi.


Hapo awali, maafisa wa Nigeria walisema sehemu za mwili wa punda - ikiwa ni pamoja na ngozi - zilisafirishwa kwa magendo hadi nchi za Asia ikiwa ni pamoja na Uchina ambako inaaminika zilitumika kutengeneza dawa za asili na vipodozi.

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu