Wagonjwa 161 waripotiwa kuugua uviko 19



Wizara ya Afya imesema idadi ya maambukizi mapya ya Ugonjwa wa Virusi vya Uviko-19 imeongezeka na kufikia 161 ikilinganishwa na maambukizi 68 kwa kipindi cha Aprili 2 hadi Mei 4, 2022.


Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na Mganga Mkuu wa Serikali, Dk Aifello Sichwale imeeleza kuwa ongezeko hilo ni sawa na asilimia 137, hali inayoashiria kuwa maambukizi yameanza kuongezeka kwa jamii.


Imeeleza katika kipindi cha miezi miwili mfululizo hakuna kifo kilichoripotiwa.


"Mchanganuo wa idadi ya waliothibitika katika kipindi cha Mei 5 hadi Juni 3, 2022 inaonesha kuwa Dar es Salaam uliripoti visa 130, Arusha (10), Mwanza (5), Shinyanga (4), Mtwara (3), Dodoma (2), Mara (2), Morogoro (1), Simiyu (1), Katavi (1), Kilimanjaro (1) na Mbeya (1), jumla ya wagonjwa watatu (3) waliothibitika kuwa na Covid-19 walilazwa na wote walikuwa hawajapata chanjo.


"Kwa takwimu hizi, inaonyesha kuwa, chanjo ni kinga dhidi ya madhara ya uviko-19, Serikali imeendelea kutoa huduma za chanjo nchini ili kuwezesha wananchi kupata kinga dhidi ya ugonjwa huu.


"Kuanzia Mei 5 hadi Mei 3 Juni 2022 jumla ya wananchi waliopata dozi kamili ya chanjo ya uviko-19 19 ni 775,680, Wizara inaendelea kuwasisitiza wananchi kupata na kukamilisha dozi za chanjo ili kuzuia kupata ugonjwa " Dk Sichwale

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu