Utafiti: Idadi ya watu yaongezeka duniani,ukuaji washukaRipoti mpya ya Umoja wa Mataifa iliyotolewa wakati dunia ikiadhimisha siku ya idadi ya watu imeeleza kwamba idadi ya watu ulimwenguni inaendelea kuongezeka lakini ukuaji unapungua.


Ripoti hiyo imesema kiwango cha ukuaji kimeshuka chini ya asilimia moja kwa mwaka katika mwaka 2020, kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1950.


Mkurugenzi wa kitengo cha Umoja wa Mataifa kinachohusika na suala la idadi ya watu John Wilmoth amesema licha ya kuweko tafauti za kikanda kuna fursa kwa nchi zinazoendelea kutokana na hali hiyo.


Amesema pamoja na kupambana na umasikini na njaa huenda pia kukaweko faida katika suala la elimu kwasababu kukiweko idadi ndogo ya watoto inamaanisha itakuwepo fursa ya mtoto mmoja mmoja kushughulikiwa zaidi.


Nchi nyingi zaidi za kipato kikubwa zitakabiliwa na upungufu wa idadi ya watu kama ambavyo inashuhudiwa hivi sasa Japan. Nchi kama Ujerumani zitahitaji kutegemea uhamiaji katika kuimarisha viwango vya ukuaji wa idadi ya watu nchini humo.

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu