Urusi yazidisha mashambulizi,kjana wa miaka 15 auawaUrusi imefanya mashambulizi mapya katika bandari muhimu ya Odessa wakati ambapo Marekani imetahadharisha kuwa Urusi inajiandaa kuzingira rasmi maeneo yanayopiganiwa kwa sasa mashariki mwa Ukraine.


Manispaa ya mji wa Odessa kupitia mtandao wa Telegram imesema shambulizi la Urusi limepiga nyumba moja iliyokuwa makaazi ya watu watano, mvulana mmoja mwenye miaka 15 akiuwawa kutokana na shambulizi hilo na msichana kulazwa hospitali kutokana na majeraha aliyoyapata.


Gavana wa eneo la mashariki la Lugansk amesema anatarajia makabiliano makali zaidi kuelekea maadhimisho ya Mei 9, siku ambayo Urusi inasherehekea ushindi ilioupata mwaka 1945 dhidi ya Wanazi wa Ujerumani.


Ila Waziri wa mambo ya nje wa Urusi Sergei Lavrov amesema majeshi ya Urusi hayatofanya mabadiliko katika uvamizi wake siku yoyote ile ikiwemo siku hiyo ya Mei 9 ambayo inaitwa Siku ya Ushindi huko Urusi.

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu