Urusi yasema haitobembeleza kuondoewa vikwazoMsemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Urusi amekiambia chombo kimoja cha ndani kuwa Moscow haitaitaka EU kuiondolea vikwazo ilivyoiwekea, licha ya kwamba Kremlin hapo awali ilieleza hatua za nchi za Magharibi kama"vita vya kiuchumi".


"Hatutafanya kama waombaji katika suala la kuondoa vikwazo."


Tuna kiwango chetu cha usalama na Umoja wa Ulaya sio kitovu cha ulimwengu"mwakilishi Nikolai Kobrinets aliiambia Ria Novosti.


Chombo cha habari cha serikali kiliripoti madai kwamba serikali ya Urusi ina mipango 100 iliyopangwa kukabiliana na vikwazo.

Siku ya Alhamisi, Urusi pia ilitishia kusitisha usambazaji wa gesi kwa nchi za nje ikiwa hawatalipwa kwa rubles.

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu