Urusi yaijibu Kenya kwa kusema kupanda kwa mafuta (Kenya) kumesababishwa na vita ya Urusi na UkraineUbalozi wa Urusi nchini Kenya umelaumu vikwazo vya nchi za Magharibi kwa kuchangia kupanda kwa gharama ya maisha katika taifa hilo la Afrika Mashariki.


Hii ni baada ya msemaji wa rais wa Kenya, Kanze Dena, kulaumu uvamizi wa Urusi nchini Ukraine kwa kupanda kwa bei ya mafuta na vyakula nchini humo.


Katika mahojiano, Bi Dena alisema kupanda kwa gharama ya maisha hakuihusu Kenya pekee.


Lakini ubalozi huo ulilaumu kupanda kwa mfumuko wa bei nchini humo kutokana na vikwazo ilivyowekewa Urusi.


"Sababu halisi ya kupanda kwa bei ya bidhaa muhimu barani Afrika sio operesheni maalum ya kijeshi ya Urusi nchini Ukraine, bali ni "vikwazo" haramu vya upande mmoja vilivyowekwa na Marekani, EU na washirika wao dhidi ya Urusi," ubalozi huo uliandika kwenye Twitter.

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu