Urusi yachekelea mauzo ya mafuta na gesi kuongezekaHuenda Urusi na rais wake Vladmir Putin wakawa wanaendelea kutimiza malengo yao baada ya kubainika kuwa mafuta na gesi yao vinauzwa kwa wingi hasa ulaya na Marekani tangu kuanza kwa vita.


Kwa mujibu wa kituo huru cha utafiti wa nishati na hewa safi (CREA), Urusi imepata takriban dola bilioni 100 kutokana na biashara ya mafuta na gesi katika siku 100 za kwanza za vita.


Hayo yamesemwa katika ripoti mpya iliyotolewa na kituo hicho.


Ripoti ya kituo hicho imesema bado kuna "mapungufu" mengi yamesalia katika umoja wa ulaya na juhudi za Marekani kupunguza uagizaji kutoka Urusi.


Umoja wa ulaya ulikuwa imepanga kwamba vikwazo vya mafuta kwa Urusi vingekuwa na athari kubwa, lakini usafirishaji wa mafuta ghafi ya Urusi kwenda India umeongezeka, wakati bidhaa za mafuta iliyosafishwa nchini India zinauzwa kwa Marekani na EU.


Kwa mujibu wa utafiti huo, asilimia 61 ya mauzo ya nje ya Urusi yalikwenda kwa Jumuiya ya Ulaya, ambayo ilinunua mafuta na gesi yenye thamani ya dola bilioni 60.


Kati ya hizo, dola bilioni 12.1 zilinunuliwa na Ujerumani na dola bilioni 7.8 na Italia.


China ilikuwa muagizaji mkubwa wa mafuta na gesi ya Urusi nje ya Uropa, na tangu Februari 24, Urusi imeuza bidhaa zenye thamani ya zaidi ya dola bilioni 12 kwa Uchina.

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu