Umoja wa Afrika wataka Sudan na Ethiopia kusitisha mapigano na kufanya mazungumzoMkuu wa Tume ya Umoja wa Afrika ameelezea wasiwasi leo kuhusu ongezeko la mzozo wa kijeshi kati ya Ethiopia na Sudan na kutoa wito kwa pande mbili kujizuwia na kufanya mazungumzo.


Matamshi hayo ya Moussa Faki Mahamat yanafuatia madai ya Sudan kwamba jeshi la Ethiopia liliwaua wanajeshi saba wa Sudan na raia moja katika tukio kwenye eneo la mpakani wiki iliyopita, madai ambayo serikali mjini Addis Ababa imeyakanusha.Sudan iliituhumu Ethiopia kwa kuwateka wanajeshi wake Juni 22 katika eneo la Al-Fashaqa, ambao ni ukanda wenye rutuba unaozozaniwa na majirani hao wawili.


Uhusiano kati ya Khartoum na Addis Ababa umezorota kuhusiana na eneo la Al-Fashaqa, lilioko karibu na mkoa wa Tigray.


Kwa muda mrefu eneo hilo limetumiwa na wakulima wa Ethiopia lakini Sudan inadai kuwa lake, na mzozo huo umekuwa ukisababisha makabiliano ya hapa na pale kati ya pande mbili, baadhi yakileta maafa.

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu