Ukraine yadai kuizamisha meli yaUkraine imedai jana kuwa imeizamisha meli kubwa ya Urusi inayobeba zana za kijeshi iliyopewa jina la Orsk.


Ukraine imesema shambulio dhidi ya meli hiyo lilitokea katika bandari inayokaliwa na Urusi ya Berdyansk.


Picha za vidio zimeonyesha moshi mkubwa ukitokea kwenye moto ulioikumba meli kubwa ya rangi ya kijivu, na kufuatiwa na mlipuko mkubwa. Urusi haikuthibitisha iwapo imeipoteza meli ya Orsk.


Shirika la habari la Urusi la TASS, limeripoti kuwa meli hiyo ilikuwa na uwezo la kubeba mizigo yenye uzito wa hadi tani 1,500.


Naibu waziri wa ulinzi wa Ukraine Hanna Malyar, amesema meli hiyo ingeweza kubeba magari 45 ya kijeshi na watu 400.


Ukraine imesema tenki la mafuta lenye ujazo wa tani 3,000 pia limeharibiwa katika shambulio hilo. Urusi iliyateka maeneo mengi ya Ukraine kwenye pwani ya bahari ya Azov.

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu