Ukraine yadai kugundua miili 1200 ya watu wasio na hatia karibu na mji mkuu wa KyivUkraine imedai kuwa imegundua miili zaidi ya watu 1,200 karibu na mkoa wa Kyiv, katika mauaji yanayodaiwa kufanywa na Urusi.


Mwishoni mwa Juma, milio ya mabomu ilisikika nchini Ukraine wakati wakaazi wa eneo la kusini wakijiandaa kwa mashambulizi mengine makali huku baadhi yao wakikimbia.


Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky kwa mara nyingine amelaani mauaji dhidi ya raia wakati alipozungumza na Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz. Viongozi hao wawili wamekubaliana kwamba wahusika wote wa uhalifu wa kivita lazima watambuliwe na kuadhibiwa.


Marekani pia kupitia mshauri wa usalama wa taifa Jake Sullivan imeapa kushirikiana na jumuiya ya kimataifa ili kuwawajibisha wahusika wa mauaji.


Naye kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis, ametoa wito wa usitishaji mapigano wakati wa sikukuu ya Pasaka ili kupisha njia kwa ajili ya amani.

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu