Uganda yathibitisha wagonjwa wapya sita vya EbolaWizara ya afya ya Uganda imethibitisha wagonjwa wapya sita wa Ebola baada ya maafisa kuthibitisha mlipuko wa ugonjwa huo nchini humo mapema wiki.


Visa hivyo vipya vya maambukizi viliripotiwa katika wilaya ya kati ya Mubende ambapo mwanamume mwenye umri wa miaka 24 alithibitishwa kufariki Jumanne baada ya kuonyesha dalili za ugonjwa huo.


Msichana wa mwaka mmoja pia anashukiwa kufariki kutokana na ugonjwa huo siku ya Jumanne.


Kati ya wagonjwa hao sita, mmoja aliripotiwa kutoka wilaya jirani.


Huu ni mlipuko wa tatu wa ugonjwa wa ebola nchini Uganda.


Zaidi ya watu 40 ambao walitangamana na familia iliyopatikana na maambukizi ya viru wamefuatiliwa.


Kumi na moja kati yao wametengwa, alisema Kyobe Henry Bbosa,kamanda wa usimamizi wa matukio kutoka wizara ya afya.

Nchi jirani zilisema ziko katika hali ya tahadhari iwapo ugonjwa huo utasambaa katika mipaka.


Wataalamu wanasema kuwa ugonjwa wa ebola Sudan kihistoria una viwango vya chini vya maambukizi na vifo ikilinganishwa na aina ya Ebola Zaire.


Mamlaka ya Uganda inaendelea kuhakikishia umma na jumuiya ya kimataifa kwamba wana uwezo wa kudhibiti janga hili.

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu