Uganda yaongoza kwa nchi zenye watu wenye furaha kuliko Kenya na TanzaniaUganda imezipiku Kenya na Tanzanzia katika tathmini ya mataifa yenye furaha Zaidi dunini .


Kenya imeshikilia nafasi ya 119 baada ya kushuka kutoka nafasi ya 86 mwaka jana huku uganda ikipiga hatuambili juu ya kenya baada ya kushuka nafasi mbili kutoka nafasi ya 83 mwaka jana .


Tanzaniaimeshuka hadi katika nafasi ya 134 ikilinganishwa na nafasi ya 94 mwaka uliotanguliwa .


Kulingana na orodha hiyo iliyotolewa na Umoja wa Mataifa Rwanda iliorodheshwa kama nchi isiyo na furaha zaidi katika kanda katika nafasi ya 143 na kuboreka kutoka nafasi ya 147.


Sudan Kusini na Burundi hazikujumuishwa katika ripoti hiyo zikiwa zimeorodheshwa katika tafiti za awali kama baadhi ya mataifa yasiyo na furaha duniani.


Kisiwa cha Mauritius kilichukua nafasi ya kwanza kama taifa lenye furaha zaidi barani Afrika kikishika katika nafasi ya 44 duniani kote.


Finland ilishika nafasi ya kwanza kama sehemu yenye furaha zaidi duniani kwa mwaka wa nne mfululizo ikifuatiwa na Denmark, Uswizi, Iceland na Uholanzi.


Orodha hiyo inaangazia vigezo tofauti ikiwa ni pamoja na vigezo vya Pato la Taifa kwa kila mtu, usaidizi wa kijamii, umri wa kuishi kiafya, uhuru, ukarimu na ufisadi.


Ingawa Kenya ina kiwango cha juu cha Pato la Taifa kwa kila mtu, nafasi yake ilishushwa na ripoti ya juu ya ufisadi

Kwa kawaida orodha hiyo hutolewa ili kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Furaha na ni sherehe ya kila mwaka inayolenga kuwasaidia watu duniani kote kutambua umuhimu wa furaha katika maisha yao.

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu