Uganda : Jeshi lakanusha madai ya kuunga mkono waasi wa TigrayJeshi nchini Uganda, limekanusha taarifa ya baadhi ya vyombo vya habari vya Ethiopia, kwamba serikali ya Uganda inaunga mkono waasi wa jimbo la Tigray, kuipindua serikali ya waziri mkuu Abiy Ahmed.


Madai hayo serikali ya Uganda kuunga mkono waasi wa TPLF yamekuwa yaripotiwa katika vyombo vya habari vya Ethiopia tangu mwezi Mei, Kwamba Uganda inawapa mafunzo waasi wa Tigray, katika eneo la Karamoja, pia kufadhili shughuli za waasi hao kupitia taifa jirani wa Sudan Kusini.


Hata hivyo msemaji wa jeshi la Uganda, UPDF, Felix Kulayigye, amesema madai serikali ya Uganda kuwa na njama kuyumbisha serikali ya Ethiopia ni ya uongo na haya msingi wowote.


Kauli ya Kulayigye, inajiri miezi kadhaa baada ya kamanda wa vikosi vya ardhini nchini Uganda, ambaye pia mwanawe rais Museveni, jenerali Gen Muhoozi Kainerugab, kuchapisha kwenye mtandao wake wa twitter taarifa zinazoashiria kuunga mkono wapiganaji wa TPLF, na tuhumu serikali ya Ethiopia kwa kukiuka haki wa binadamu.


Kutokana na tuhuma hizi, mwezi Mei mwaka huu, waziri wa ulinzi wa Uganda Vincent Ssempijja, alilazimika kusafiri kuenda nchini Ethiopia, ambapo alikutana na mkuu wa jeshi nchini humo Birhanu Jula, wakidaiwa kujadili maswala ya usalama, ikiwemo tuhuma za serikali ya Uganda kuingilia usalama wa Ethiopia.

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu