Uefa kuanzisha mashindano ya wakimbiziUEFA imetangaza kuanza kwa mashindano mapya ya Kimataifa ya soka kwa wakimbizi "Unity Euro Cup" mwishoni mwa mwezi huu.


Mashindano hayo yatahusisha timu 8. Asilimia 70 ya timu hizo zitakuwa na wachezaji ambao ni wakimbizi na asilimia 30 wasio wakimbizi.


Mashindano hayo yatafanyikia katika mji wa Nyon nchini Uswisi ambako ndiko yalipo makao makuu ya UEFA.


Unity Euro Cup ni mashindano ya kirafiki na yatahusisha timu kutokea Austria, Belgium, Germany,France,Italy, Malta, Ireland na Switzerland.


Dhumuni la mashindano hayo ni kuimarisha uhusiano kati ya wakimbizi na jamii walizohamia kwa kupitia nguvu ya soka.


Tangazo la mashindano hayo limetolewa rasmi katika siku ya wakimbizi duniani Juni 20.

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu