Tetetmeko laua watu elfu moja AfhganistanTetemeko kubwa la ardhi limepiga eneo la vijijini la milima ya mashariki mwa Afghanistani mapema leo, na kusababisha vifo vya watu 1,000 na kuwajeruhi wengine 1,500, likiwa moja ya matetemeko mabay azaidi katika miongo kadhaa, huku maafisa wakionya kwamba idadi ya vifo huenda ikaongezeka.


Kumekuwepo na taarifa chache kuhusu tetemeko hilo lenye ukubwa wa 6.1 kwenye kipimo cha richter, lililotokea karibu na mpaka wa nchi hiyo na Pakistan.


Janga hilo limeuweka katika mtihani mkubwa utawala wa kundi la Taliban, ambalo lilitwaa madaraka mwaka uliopita baada ya Marekani kuondoa wanajeshi wake nchini humo na kumaliza vita vyake vilivyodumu kwa muda mrefu zaidi, miongo miwili baada ya kuwaondoa madarakani waasi hao kufuatia mashambulizi ya Septemba 11, 2001.


Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Masuala ya Kiutu - OCHA imesema inafanya kila liwezekanalo kutengeneza makaazi ya dharura, vituo vya ushauri na kutoa msaada wa chakula katika eneo lililoathirika na tetemeko hilo la ardhi.


OCHA imesema washirika wa kiutu wanajiandaa kuzisaidia familia zilizoathirika katika mikoa ya Paktika na Khost, kwa ushirikiano na mamlaka za Taliban.

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu