Tahadhari,penseli,mabegi vinatumika kuunga mkono mapenzi ya jinsia mojaMamlaka nchini Saudi Arabia imekuwa ikivikamata vinyago vya rangi ya upinde wa mvua na mavazi ya watoto, ambayo wanadai yanashinikiza mapenzi ya jinsia moja TV ya serikali inasema.


Ripoti ya kituo hicho cha televisheni cha Al-Ekhbariya ilionyesha maafisa wa wizara ya biashara wakiondoa bidhaa mbalimbali kutoka kwa maduka katika mji mkuu wa Riyadh.


Zilijumuisha klipu za nywele, pop-its, t-shirt, kofia na mifuko ya penseli.Afisa mmoja alisema bidhaa hizo "zinakinzana na imani ya Kiislamu na maadili ya umma, na kukuza rangi za wapeinzi wa jinsi moja ".


Wizara ya biashara ilituma ujumbe wa tweeter kwamba maafisa wake walikuwa wakichukua "bidhaa ambazo zina alama na ishara zinazotaka kupotosha".Maduka yatakayopatikana yakiuza yatakabiliwa na adhabu za kisheria, iliongeza.

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu