Sita wauawa kwa risasi kwenye shambulizi la holela MarekaniWatu sita wameuawa na wengine tisa kujeruhiwa kwa risasi katika mji mkuu wa jimbo la California wa Sacramento mapema leo Jumapili.


Polisi wamesema shambulio hilo limetokea katika eneo lenye migahawa mingi.


Video iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii imeonyesha watu wakizozana barabarani, kisha kuanza kukimbia huku milio ya risasi ikisikika.


Hili ni tukio la hivi karibuni la mauaji ya watu wengi nchini Marekani, ambapo bunduki husababisha takribani vifo 40,000 kwa mwaka kulingana na tovuti inayorekodi ghasia za bunduki ya Gun Violence Archive.


Robo tatu ya mauaji yote nchini Marekani hutokana na mashambulizi ya bunduki huku idadi ya bastola na bunduki nyingine zinazouzwa ikiendelea kuongezeka. Mwaka 2020 zaidi ya bunduki milioni 23 ziliuzwa nchini humo.

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu