Simba yamtakia kila la kheri Morison,yachanganya mashabiki

Klabu ya Simba imempa mapumziko ya hadi mwisho wa msimu mchezaji wake Bernard Morrison.


Simba imefikia maamuzi hayo baada ya pande zote mbili kukubaliana kwa lengo la kumpa nafasi Morrison kupumzika na kushughulikia mambo yake binafsi.


Simba inamshukuru Morrison kwa mchango wake kwa kipindi chote alichohudumu ndani ya klabu yetu.


Tunatambua na kuthamini mchango wa Morrison katika miaka miwili aliyoitumikia klabu yetu na kuisadia kupata mafaniko kadhaa ikiwemo kucheza robo fainali ya michuano ya Afrika mara mbili, kuchukua ubingwa wa ligi kuu Tanzania bara, ubingwa wa kombe la shirikisho la Azam Sports, na ubingwa wa kombe la Mapinduzi.


Kwa mchango na mafanikio hayo klabu inamshukuru mchezaji huyo kipenzi cha wanasimba kwa kujitoa kwake kuipigania klabu yake.


Simba inamtakia kila la heri Bernard Morrison katika mapumziko yake na safari yake ya soka hapo baadae.

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu