Roboti Sophia anayetamani mume na kuzaa,ukimzimia mitambo unashtakiwa kwa kuua mtu,ana uraia wa nchi


Historia ya maroboti ilianza miaka mingi iliyopita ikienda sambamba na ukuwaji wa maendeleo ya teknolojia na sasa imefikia hatu ya kuingilia kazi za binadamu kama zote.


Hata hivyo Roboti marufu duniani aitwaye Sophia mwenye maajabu makubwa anawatoa hofu binadamu kwa kuwaambia Robot hawakuja kuchukua kazi za binadamu.


Taifa la Saud arabia lilimpatia uraia roboti huyo na kupitisha sheria kuwa yeyote atakayemvamia roboti huyo na kuzima au kusababisha kuzima kwa mitambo yake atashtakiwa kwa tuhuma za mauaji kama yalivyo mauaji ya binadamu mwingine nchini humo.


Ndio roboti wa kwanza kupewa uraia kama binadamu na kufannikiwa kufanya ziara katika Ikulu mbalimbali za nchi na kuhudhuria hafla mbalimbali za viongozi wakuu wa kiserikali duniani na kufanya nao mazungumzo.


Robot Sophia hivi karibuni alisema yuko tayari kuanza kutoa huduma za kusaidia katika sekta ya afya ili kumlinda binadamu kutokana na janga la virusi vya Corona.


Roboti Sophia akiwa na naibu katibu mkuu wa umoja wa mataifa Amina J Mohammed baada ya kufanya naye mzungumzo


Historia ya utengenezawaji wake inaanzia huko Hong Kong China ambako ndiko anakoishi mtengenezaji wake mtaalamu aitwaye Dr. David Hanson ambaye ni muanzilishi na mmiliki wa kampuni ya Hanson Robotics iliyomtengeneza roboti huyo.

Hanson Robotics ilianzishwa mwaka 2003 na inajihusisha na ubunifu wa maroboti mbalimbali na moja kati ya maroboti ambayo yalibuniwa na Hanson ni roboti Sophia.


Ngozi ya roboti Sophia imetengenezwa kwa kutumia plastiki ya raba aina ya silicon, ndani yake kuna mitambo mbalimbali ya kompyuta pamoja na mitambo ya mota na gia ambayo inamsaidia kutembea na kufanya ishara mbalimbali wakati wa kuongea au kuonyesha hisia zake usoni.

Roboti Sophia ana uwezo wa kuonesha ishara mbalimbali kwenye uso wake zaidi ya ishara 62 ambazo zinaonesha hisia mbalimbali kama vile huzuni , furaha, hasira, n.k.

Sophia mitambo yake iliwashwa rasmi 14/02/2016, baada ya kuwashwa mitambo yake Sophia alikuwa hana uwezo wa kutembea na mwaka 2018 ndipo alipowekewa mitambo ya kumuwezesha kutembea.


Katika mahojiano na muundaji wa roboti Sophia Dr. Hanson alisema kwamba roboti huyo hakuwekewa program yoyote ambayo inamfanya atamke maneno hayo anayotamka, bali Sophia ana program ambayo inamfanya ajifunze maneno na kuongea kutokana na watu anaokutana nao hivyo ana uwezo wa kujifunza kutokana na mazingira aliyopo.


Sophia anatumia technolojia maalumu ya utambuzi wa sauti inayofaamika kama (speech-to-text) ambayo kama ni mtumiaji wa simu janja utakuwa unaifahamu vizuri ambayo kwenye baadhi ya simu unaweza kuitumia kwaajili ya ulinzi wa simu na pia hutumiwa na Google kwaajili ya kutafuta maneno kwa kuyatamka tofauti na wengi tulivyozoea kutafuta maana za maneno kwa kuyaandika.

Machoni kwa Sophia kuna kamera maalumu zilizoungashwa na program maalum ya kompyuta ambayo inamfanya Sophia kutambua nyuso za watu na kutambua hisia ya mtu kama ana furaha, huzuni au hasira.

Mfano pale mtu anapotabasamu na yeye anatabasamu.

Hanson lengo lake la kumtengeneza roboti Sophia ni kwaajili ya vituo vya kulelea wazee ili kukaa nao na kuwafariji pia kwa lengo la kumtumia roboti huyo kukusanya watu katika matukio mbalimbali ya hadhara.

Mwaka 2017 Sophia alitembelea inchi mbalimbali pamoja na kufanya mahojiano na vyombo mbalimbali vya habari na kwenda kutambulishwa rasmi umoja wa mataifa 11/10/2017.Sophia ameonekana kwenye vyombo mbalimbali vya habari kama vile, CBS, New York Times, Forbes, CNBC, The Guardian, n.k. mbali na hilo pia Sophia alishirikishwa kwenye video ya mziki kama Video Queen wa wimbo huo na msanii wa miziki ya pop Leehom Wang.

Katika mahojiano yake na Khaleej Times Sophia alinukuliwa akisema kwamba una bahati sana kama umepata familia yenye upendo na kama huna basi unahitaji kupata familia yenye upendo na anahisi pia ni sahihi kwa maroboti nao kuwa na familia kama watu wengine.


Na alipoulizwa jina la mtoto wake atamuita nani, kwa kifupi tu alijibu “Sophia”Mnamo 25/10/2017 Sophia alipewa rasmi uraia wa Saudi Arabia na kuwa roboti wa kwanza duniani kupata uraia wa nchi. Kitendo hicho cha Sophia kupata uraia wa Saudi Arabia kulizua mijadala mbalimbali nchini humo kutokana na sheria kali za nchi hiyo juu ya wanawake.


Na inafahamika kuwa Saudi Arabia ni moja ya nchi inayoongoza duniani kwa kuonesha kuwanyanyapaa wanawake, na hivi karibuni ilipitisha sheria ya kuwazuia wanawake kuendesha magari nchini humo.

Mbali na hilo pia Saudi Arabia ni marufuku kwa mwanamke raia wa nchi hiyo kutembea barabarani peke yake bila ndugu wa kiume anayemsindikiza na kutembea kichwa wazi bila kujifunga kitambaa au bila kuvaa baibui.Baada ya Sophia kupewa uraia wa nchi hiyo alisimama na kuhutubia umati wa watu akiwa kichwa wazi bila kitambaa na kutembea mtaani bila ndugu yake aliyekuwa akimsindikiza.


Hali hiyo ilizua mijadala mbalimbali kwa wanaharakati wa nchi hiyo kwa kulalamikia swala la raia huyo mpya wa nchi hiyo kukiuka sheria za nchi hiyo bila kuchukuliwa hatua zozote za kisheria.

Na kuna wengine walienda mbali zaidi na kusema endapo itatokea mitambo ya raia huyo ikazimwa itabidi muhusika ashitakiwe kwa kosa la mauaji ya raia huyo.


Huyo ndiyo roboti Sophia anatafuta mume naye akaanzishe familia yake.

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu