Rais Samia ataja sababu kushiriki ‘The Dream Concert’, ya SuguRais Samia Suluhu Hassan ametaja sababu za kukubali kushiriki kwenye tamasha la msanii wa muziki wa HipHop, Joseph Mbilinyi maarufu Sugu ‘The Dream Concert’ huku akizindua kitabu cha muziki na maisha cha mwanamuziki huyo.


Tamasha hilo limefanyika usiku wa kuamkia leo Jumatano Juni Mosi kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam likiwa ni maalumu kwa mbunge huyo wa zamani wa Mbeya Mjini kuadhimisha miaka 30 kwenye sekta ya muziki.


Akieleza sababu ya kukubali kushiriki tamasha hilo, mkuu huyo wa nchi ameweka wazi sababu mbili akisema "Kwanza kwa Joseph mimi ni mama hivyo niliona fahari kushuhudia mafanikio ya mwana”


Akitaja sababu ya pili, Rais Samia amesema "Lakini pia nilivutiwa na wazo la kuandika kitabu, nikasema naenda kumsapoti, japo tarehe aliyoipanga mwanzo nilikuwa bize, akasema atasogeza mbele na leo niko hapa na nitazindua kitabu chake," amebainisha


Akitaja majina ya utani ya mwanamuziki huyo likiwamo la Taita na Sugu ambalo alisema hawezi kumuita kwa kuwa sasa mwanamuziki huyo huku akikumbusha moja ya tukio la Sugu lililotokea bungeni wakati mkali huyo wa HipHop akiwa anawawakilisha wananchi wa Jimbo la Mbeya Mjini.


"Mimi nitamuita Joseph, nakumbuka siku alipomuudhi Spika akasema mtoeni nje, alishikwa mguu na mkono," amesema Rais Samia.


Amesema safari ya Sugu kwenye tasnia muziki haikuwa rahisi, aliingia wakati bado muziki ukiwa haukubariki.


Katika tamasha hilo, Rais Samia aliweka wazi kuwa kuna kipendi hata yeye alikuwa mtazamo kuwa mziki wa HipHop ni uhuni huku akieleza kuwa mtazamo huo umebadilika.


"Hata mimi nilipokuwa nikiwaona wanafoka foka niliona uhuni wakati ule, lakini kumbe sio kweli, muziki umeleta heshima," amesema.


Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu