Rais Samia akataa ombi la kuipandisha hadhi MbaliziRais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema Serikali yake haina mpango wa kukata maeneo kwa kuyapandisha hadhi, badala yake wanajielekeza kwenye utatuzi wa shida za wananchi hapa nchini.


Rais Samia ametoa msimamo huo leo Ijumaa Agosti 5, 2022 akiwa Mbalizi mkoani Mbeya baada ya kupokea ombi kutoka kwa mbunge wa Mbeya Vijijini, Oran Njeza la kutaka Mbalizi kupandishwa hadhi na kuwa halmashauri ya mji.


Mbunge huyo alimwomba Rais Samia kuupandisha hadhi mji wa Mbalizi ili uwe halmashauri ya mji akidai kwamba itasaidia kusogeza huduma za kijamii kwa wananchi wa Mbalizi na maeneo mengine ya jirani.


Akizungumzia jambo hilo, Rais Samia amesema alipokea ombi hilo kutoka kwa viongozi, hata hivyo amewaeleza wananchi wa Mbalizi kwamba Serikali yake imejielekeza kwenye utatuzi wa shida za wananchi.


“Nilipofika uwanja wa ndege, mkuu wa mkoa na mbunge waliniambia kuhusu halmashauri nikawaambia, halmashauri maana yake ni gharama zaidi, viongozi zaidi, mishahara zaidi, magari zaidi, gharama kwa Serikali, majengo zaidi, gharama kwa serikali.”


“Kwa sasa hivi, wananchi wangu wa Tanzania wana shida chungu nzima, wanataka umeme, wanataka madarasa. Mwaka jana tulijenga madarasa 15,000 sekondari na mengi katika shule za msingi.

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu