Rais Samia afanya uteuzi huu Muhimbili, akiwa LondonRais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amemteua Profesa Mohamed Janabi kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), akichukua nafasi ya Profesa Lawrence Maseru ambaye amestaafu.


Uteuzi wa Profesa Janabi ambaye alikuwa mkurugenzi Mtendaji wa wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), umetangazwa jana Jumapili Septemba 18, 2022 na kupitia taarifa ya Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu Zuhura Yunus.

Uteuzi huo umefanyika wakati Rais Samia akiwa London nchini Uingereza kuhudhuria mazishi ya Malkia Elizabeth II yanayofanyika leo Jumatatu.

Katika uteuzi huo, nafasi ya Profesa Janabi imechukuliwa na Dk Peter Kisenge aliyetuuliwa kuwa mkurugenzi mtendaji wa JKCI. Hata hivyo uteuzi wao utaanza Oktoba 2 mwaka huu.

Profesa Janabi aliteuliwa mwaka 2016 na aliyekuwa Rais wa awamu ya tano, Hayati John Magufuli.Kabla ya kuteuliwa Profesa Janabi alikuwa daktari mkuu binafsi wa rais mstaafu Jakaya Kikwete.

Kabla ya uteuzi huo, alikuwa akikaimu nafasi hiyo toka kuanza rasmi kazi kwa taasisi hiyo Septemba mwaka 2015

Vivyo hivyo, kwa Profesa Maseru aliteuliwa na hayati Magufuli mwaka 2016, kabla ya hapo alikuwa akikaimu nafasi hiyo.

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu