Rais Samia aahidi kuimalizia miradi yote iliyonzishwa wilayani Chato kumuenzi Rais MagufuliRais SamiaSuluhu Hassan ameahidi kukamilisha miradi yote iliyoanzishwa na mtangulizi wake hayati rais John Pombe Magufuli .

Katika hotuba yake ya kumbukizi ya mwaka mmoja tangu kifo cha rais huyo wa awamu ya tano rais Samia alieleza yote ambayo mtangulizi wake aliyaenzi kama vile kuhakikisha nchi inajitegema na kupigana na rushwa.


‘'Nitaendeleza mema yote aliyotuachia Magufuli na kuleta mema mapya'’ rais Samia amesema


Aliitaja baadhi ya miradi iliyokamilika ambayo ilianzishwa na hayati Magufuli ikiwemo

daraja la Tanzanite jijini Dar-es-salaam na jitihada za kuboresha na kuendeleza huduma za maji ikiwemo afya,elimu na umeme.


Rais Samia pia aliwahakikishia wenyeji wa Chato kwamba miradi yote iliyoanzishwa Chato itakamilishwa


‘'Ujenzi wa kivuko cha Chato umeshakamilika kwa asilimia 100 na ujenzi wa kiwanja cha ndege cha chato kipo kwa asilimia 95.


Miradi hii itakapokamilika nitakuja kuifungua mwenyewe kama angevyofanya rais Magufuli’ rais Samia alisema.

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu