Rais amteua Wambura kuwa IGP mpyaRais Samia Suluhu Hassan wa jamhuri ya muungano wa Tanzania amempandisha cheo Kamishna wa Polisi, Camillus Wambura na kumteua kuwa Inspekta Jenerali na Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania (IGP). Wambura alikuwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI).


Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Jumatano Julai 20, 2022 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Zuhura Yunus imeeleza kuwa Rais amemteua aliyekuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi, Simon Sirro kuwa Balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe.


Rais Samia Suluhu Hassan amempandisha cheo Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Ramadhan Kingai kuwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI). Kingai anachukua nafasi ya Camillus Wambura ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania (IGP).

Julai 15 mwaka huu, taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini, David Misime ilisema kuwa Kingai amehamishwa kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma akitokea Mkoa wa Kinondoni.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Jumatano Julai 20, 2022 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Zuhura Yunus imeeleza kuwa Kingai anachukua nafasi ya Wambura ambaye ameteuliwa kuwa IGP.

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu