Putin: Nchi za Magharibi haziwezi kususia nishati ya UrusiRais wa Urusi Vladimir Putin anasema nchi za Magharibi hazitaweza kususia mafuta na gesi ya Urusi kwa miaka kadhaa.

Aliongeza kuwa hakuna mtu anayejua nini kinaweza kutokea wakati huo, kwa hivyo kampuni za Urusi hazitakuwa "zikitengeneza visima vyao vya mafuta".


Haya yanajiri wakati afisa wa Marekani amekiri kwamba faida ya nishati ya Urusi inaweza kuwa juu sasa kuliko ilivyokuwa kabla ya vita.


Muungano wa Ulaya( EU) kwa sasa unaagiza karibu asilimia 40 ya gesi yake kutoka Urusi.


Muungano huo umeahidi kupunguza utegemezi wake kwa mafuta ya Urusi kwa asilimia 90 ifikapo mwisho wa 2022, lakini hadi sasa haujatoa ahadi yoyote juu ya gesi.


Marekani imeweka vikwazo dhidi ya bidhaa zote za nishati za Urusi. Vikwazo hivyo vimewekwa kwa lengo la kuadhibu Moscow kwa kuivamia Ukraine.


Lakini kupanda kwa bei ya mafuta na gesi duniani kunamaanisha kwamba faida ya Urusi inaweza kuongezeka katika miezi ya hivi karibuni, licha ya kupunguzwa kwa usambazaji wa jumla."Kiasi cha mafuta kinapungua katika soko la dunia, bei inapanda," Rais Putin aliambia kundi la wajasiriamali vijana.

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu