Putin awajibu viongozi wa ulaya waliombeza kubaki kifua waziRais wa Urusi Vladimir Putin amewajibu viongozi wa nchi za ulaya ambao walikejeli picha zake za kifua wazi wiki hii akiwaambia "itakuwa ni kituko endapo na wao watabaki kifua wazi kama yeye.


Matamshi hayo yametolewa baada ya viongozi katika mkutano wa G7 kukejeli tabia ya rais wa Urusi kuonekana kifua wazi katika picha tofauti.


Akijibu shutma hizo rais Putin amewashauri viongozi wenzake hao wa nchi kuacha kunywa pombe kupitiliza na badala yake wajihusishe na mazoezi kwakuwa wao wakibaki kifua wazi kama yeye watachekesha.


"Ili kila kitu kiwe sawa, lazima uache kutumia pombe vibaya na maovu mengine,badala yake ni kufanya mazoezi, kucheza michezo mbalimbali." alisema Putin


"Wenzetu nawafahamu wote binafsi , hatuko kwenye kipindi bora cha mahusiano yetu, hilo linaeleweka," aliongeza.Putin aliongeza kuwa "Lazima ujitunze, na ukweli kwamba wanaozungumza juu yangu ni vizuri sana, ninawapongeza kwa hilo."


Pia alikemea maoni ya Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson, ambaye alisema kuwa Putin hangeivamia Ukraine ikiwa angekuwa mwanamke.


Wakati wa mkutano na waandishi wa habari, Putin alisema kuwa tathmini hii "si sahihi" na akasema kwamba Margaret Thatcher "aliamua kuanzisha uhasama" katika Vita vya Falklands/Malvinas.


Wakati maoni ya Putin yaliporipotiwa kwa Boris Johnson wakati wa mkutano wa waandishi wa habari wa NATO siku ya Alhamisi, waziri mkuu wa Uingereza hakujibu moja kwa moja, lakini badala yake aliangazia jinsi mataifa ya Magharibi yalivyokusanyika katika kukabiliana na uvamizi wa Ukraine.

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu