Polisi wa A.Kusini kupita baa kwa baa baada ya vijana 21 kufariki


Polisi wa Afrika Kusini wameripotiwa kuwa wataanza kufanya uchunguzi wa baa kwa baa na sehemu za sterehe ili kujua usalama wa maeneo hayo na tahadhari zinazochukuliwa wakati wa hatari.


Siku ya Jumatatu askari polisi nchini humo walikuwa wakifanya uchunguzi katika klabu ambapo vijana 21 walifariki kwa njia isiyoeleweka huku manusura wakielezea vita vya kutoroka eneo lililokuwa limejaa msongamano wa watu huku mtu mmoja akisema kulikuwa na ukosefu wa hewa safi.


Wengi wa waathirika, wengine wakiwa na umri wa miaka 13, walipatikana wamefariki ndani ya baa maarufu katika jiji la kusini mwa London Mashariki.


11 walifariki dunia ndani ya baa hiyo, huku wanne wakifia hospitalini.Wengine 31 walilazwa hospitalini wakiwa na dalili zikiwemo maumivu ya mgongo, vifua kubana, kutapika na maumivu ya kichwa, afisa alisema.


Wengi waliruhusiwa kuondoka hospitali siku ya Jumapili huku wengine wawili wakisalia hospitalini, walisema.


Bw Cele, ambaye alitembelea eneo la tukio na kupewa taarifa na polisi wa eneo hilo, alisema waliofariki walikuwa na umri wa kati ya miaka 13 na 17 - lakini orodha ya kina ya wahasiriwa wakati huo haikuwa imetolewa.Umri wa chini wa kisheria wa kunywa pombe nchini Afrika Kusini ni miaka 18.

Kuna ripoti kwamba watu waliokuwa wameenda kujivinjari walikuwa wakisherehekea mwisho wa mitihani ya shule.

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu