Polisi Denmark wasema ukio la mauaji kwa risasi sio la kigaidiPolisi nchini Denmark imesema leo kuwa watu wanne wako katika hali mahututi baada ya kupigwa na risasi katika eneo moja la maduka mjini Copenhagen hapo jana ambapo watu watatu waliuawa.


Mkuu wa polisi Soren Thomassen amewaambia waandishi habari hakuna dalili kuwa shambulizi hilo ni kitendo cha ugaidi au kuwa mshukiwa huyo alifanya shambulizi hilo kwa ushirikiano na wengine.


Amesema mshukiwa huyo aliwauwa watu wawili wenye umri wa miaka 17, mwanamme na mwanamke, na raia mmoja wa Urusi mwenye umri wa miaka 47 anayeishi Denmark.


Mshukiwa huyo, ambaye polisi imesema alikuwa kwenye rekodi za madaktari wa afya ya akili nchini Denmark, alikuwa na bunduki, risasi na kisu wakati alipokamatwa. Atafikishwa mahakamani baadae leo.


Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu