Papa awaombea wahasiriwa wa shambulio la kanisa la NigeriaPapa Francis amewaombea wahanga wa shambulizi dhidi ya kanisa moja nchini Nigeria ambapo waumini wasiopungua 25 waliuawa na watu wenye silaha.


Taarifa ya Vatican ilisema amefahamu kuhusu vifo vya makumi ya watu. Shambulio hilo lilifanyika katika mji wa kusini wa Owo, katika jimbo la Ondo.Maafisa huko wameonya kwamba idadi ya waliojeruhiwa inaweza kuongezeka.


Wanasema kasisi mmoja na washiriki wengine wa kanisa hilo walitekwa nyara na watu hao wenye silaha, ambao hawakujulikana ni nani.


Rais wa Nigeria, Muhammadu Buhari, amelaani shambulio hilo na kulitaja kuwa la "chuki".


Wiki moja iliyopita, mkuu wa kanisa la Methodist nchini humo alitekwa nyara na aliachiliwa huru baada ya kulipwa fidia.

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu