Pacha mmoja aliyetenganishwa Muhimbili afarikiMmoja kati ya watoto pacha waliotenganishwa Julai Mosi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Neema amefariki dunia wakati akiendelea na matibabu Jumapili Julai 10, 2022.


Taarifa iliyotolewa na Hospitali hiyo leo Julai 12, 2022 na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano kwa Umma, Aminiel Aligaesha imeeleza kuwa hali ya Neema ilibadilika ghafla akiwa katika chumba cha wagonjwa mahututi (ICU).


Muhimbili ilifanikisha upasuaji wa kuwatenganisha watoto hao walioungana kifuani Rehema na Neema Julai 1 mwaka huu.


Katika taarifa yake, Aligaesha amesema “Nasikitika kukufahamisha kuwa mtoto Neema ambaye alitenganishwa na mwenzake Rehema amefariki jumapili ya Julai 10 saa 3 asubuhi.


“Akiwa ICU hali yake ilibadikika ghafla, madaktari walijitahidi kurudisha hali yake bila mafanikio na hatimaye kupoteza maisha. Twendelee kumwombea Rehema ambaye bado yupo ICU ili Mwenyezi Mungu amjalie afya njema. Bwana alitoa na Bwana ametoa, jina lake lihimidiwe sana,” ameeleza


Bibi wa Pacha hao Dorica Josiah amesema amepokea taarifa hiyo kwa masikitiko makubwa kwani hali ya watoto hao ilikuwa inaimarika tangu walipofanyiwa upasuaji.

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu