Ofisi ya mwendesha mashitaka yamchunguza aliyekuwa rais Enrique Peña NietoOfisi ya mwanasheria mkuu wa Mexico imesema Jumanne kuwa inamchunguza Enrique Peña Nieto, ambaye alitawala nchi hiyo kati ya mwaka 2012 na 2018.


Anashukiwa kwa uhalifu ikiwa ni pamoja na kujitajirisha haramu na utakatishaji fedha.


Rais wa zamani wa Mexico anakabiliwa na tuhuma kashfa mbalimbali na vyombo vya sheria. Ofisi ya mwanasheria mkuu wa Mexico ilitangaza Jumanne, Agosti 2, kwamba inamchunguza Enrique Peña Nieto kwa tuhuma za kujitajirisha haramu, utakatishaji fedha, pamoja na uhalifu wa uchaguzi na ufujaji wa mali za umma.


Tangazo hilo linakuja karibu mwezi mmoja baada ya ripoti kutoka kitengo cha Ujasusi wa Fedha cha Wizara ya Fedha kusema rais wa zamani Enrique Peña Nieto alipokea zaidi ya dola milioni moja kupitia uhamisho usio halali na kudumisha 'mahusiano' na makampuni yaliyoshinda kandarasi kubwa za serikali chini ya uongozi wake.


Moja ya uchunguzi ulofunguliwa unahusu "malalamiko mbalimbali ambapo kampuni ya ujenzi ya Uhispania OHL inahusika", ofisi ya mwendesha mashtaka wa umma ilisema katika taarifa siku ya Jumanne bila kutoa maelezo zaidi.


"Katika uchunguzi huu, hatua iliyofikiwa itawezesha kuanzisha kesi katika miezi ijayo," ofisi hiyo ilisema.


Nia ya AMLO ya kupiga vita ufisadi


Rais huyo wa zamani, ambaye alikuwa madarakani toka mwaka 2012 hadi 2018 na sasa anaishi Madrid, alijibu shutuma hizo mnamo mwezi Julai, akikana hatua zozote zisizo halali. Alisema najiandaa kuweka wazi maswali yoyote kuhusu mali (zake) na kuonyesha uhalali" wa mali hizo.


Rais wa mrengo wa kushoto wa Mexico Andrés Manuel López Obrador (AMLO), ambaye alimrithi Enrique Peña Nieto mnamo 2018, amekuwa akiwashutumu watangulizi wake mara kwa mara kwa ufisadi.


Mnamo mwezi wa Agosti 2021, kura ya maoni ambayo alikuwa ameitaka iwapo achunguze na kuwashtaki watangulizi wake kwa madai ya ufisadi ilikuwa na idadi ndogo ya waliojitokeza, mbali na akidi inayohitajika.

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu