Njaa inavyotesa na kuua raia Ethiopia kisa vita vya wenyewe kwa wenyewe
Tathmini mpya ya uhakika wa upatikanaji wa chakula iliyotolewa mwishoni mwa mwezi Januari 2022 na Shirika la Umoja wa Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula la Umoja wa Mataifa WFP, inaonesha takriban asilimia 40 ya wakazi wa Tigray Ethiopia wanakabiliwa na ukosefu mkubwa wa chakula ikiwa ni miezi 15 ya migogoro kaskazini mwa Ethiopia.


Utafiti wa WFP ulibaini asilimia 13 ya watoto wa Tigray walio chini ya miaka 5, nusu ya wanawake wote wajawazito na wale wanaonyonyesha wana utapiamlo, hivyo kusababisha matokeo mabaya ya ujauzito, uzito mdogo, udumavu na vifo vya uzazi.


Adrian Van Der Knaap, Naibu Mkurugenzi wa WFP nchini Ethiopia anasema inakadiria kwa wastani, familia zilizoathiriwa na mzozo kaskazini mwa Ethiopia zilikuwa zikipata chini ya asilimia 30 ya mahitaji yao ya kalori katika miezi iliyopita, na kwamba uhitaji wa chakula utaendelea kwa mwaka mzima wa 2022, “migogoro inaendelea kusababisha njaa zaidi na zaidi. Tuna watu milioni kadhaa huko Tigray katika hali mbaya sana, mamia ya maelfu ya watoto wenye utapiamlo sana huko Afar, huko Amhara pia hali sio nzuri. Kwa jumla zaidi ya watu milioni 9 hawana chakula kwa sasa.”


WFP imetoa ombi la msaada wa dola milioni 337 kusaidia wakazi wa Kaskazini mwa Ethiopia katika kipindi cha miezi sita ijayo. Na katika nchi ya Ethiopia ina pengo la ufadhili ambalo halijawahi kushuhudiwa la dola milioni 667 ili kuweza kubadili maisha ya watu milioni 12 katika kipindi cha miezi sita ijayo.


Video moja iliyotolewa na shirika la WFP inamuonesha mjamzito mmoja raia wa Ethiopia Bi Hiwot, mama wa watoto wanne akiwa na binti yake ambaye awali alikuwa na utapiamlo lakini msaada wa chakula chenye lishe kutoka WFP umemsaidia sasa kuwa na hali nzuri. Mama huyu anaeleza kuwa hata yeye anategemea usaidizi wa lishe ya WFP katika kipindi chote cha ujauzito wake kwani familia yake inaishi kwa chai “kwa sababu ya uhaba wa chakula tunawapa watoto wetu kwanza na ikiwa kuna kitu chochote kimebaki ndio tunaweza kula. Vinginevyo, tunaenda kulala tumbo likiwa tupu. Ingawa mimi ni mjamzito sijapata mlo kamili.”


Ethipoia imekuwa katika mapigano na kundi la Tigray Peoples Liberation Front (TPLF) linalopingana kwa kiasi kikubwa na rais wa taifa hilo Abiy Ahmed.


KUmekuwa na taarifa kuwa serikali imekuwa ikizuia magari ya kutoa misaada kwa watu wa Tigray kiasi cha kumuibua mara kwa mara mkuu wa shirika la afya duniani Tedros Adhanom Ghebreyesus ambaye pia ni Raia wa taifa hilo akiitupia lawama serikali.


Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu