Ni lazima kwa Liberia wanawake kunyonyesha watoto kwa miezi 6Bunge la Libeŕia kwa kauli moja limepitisha mswada unaowataka akina mama kunyonyesha watoto wao kwa angalau miezi sita.


Mwakilishi wa Wilaya ya Rivercess Country #2 Byron W. Zahwea mnamo 2021 alipendekeza sheria ili kuhakikisha kwamba uuzaji wa bidhaa ambazo ni mbadala wa maziwa ya mama unadhibitiwa ipasavyo ili kuepuka uagizaji na uuzaji wa vitu ambavyo vinaweza kuathiri watoto wachanga.


Bunge hilo, wakati linapitisha mswada wa 'Kunyonyesha, Udhibiti na Chakula cha Watoto', lilisema kuwa ni haki ya kila mtoto kunyonyeshwa kwa miezi sita na kwamba muswada huo umeundwa kusaidia "kukuza uhusiano mzuri kati ya mama na mtoto’.


“Kunyonyesha ni sehemu muhimu ya maisha ya mwanadamu duniani na kwamba maziwa ya mama, pamoja na mambo mengine, yana virutubishi vilivyo katika uwiano unaofaa, ambavyo ikibidi kubadilishwa, vifanywe na kitu ambacho kinatumika kwa madhumuni sawa na maziwa ya mama kwa kuzingatia kwamba ni muhimu kwa uingizwaji wa maziwa ya mama wakati kuna hali ya kiafya au hali zingine zinazotishia maisha ya mtoto mchanga au mtoto mdogo,” marekebisho hayo yanasisitiza.


Mwaka 2020, UNICEF iliripoti kuwa watoto 5 kati ya 10 nchini Libeŕia wanapata maji ya kawaida, vivywaji vingine, na vyakula pamoja na maziwa ya mama wakati wa miezi sita ya kwanza ya maisha yao, na hivyo kuchangia utapiamlo wa watoto, magonjwa na hata kifo.


Kulingana na ripoti ya 2020, inagharimu Liberia dola za Kimarekani 200,000 kila mwaka kutibu watoto wenye ugonjwa wa kuhara na nimonia, na kisukari cha aina ya II kwa akina mama wanaotembelea vituo vya afya kutokana na kutonyonyeshwa kwa muda wa kutosha.


"Liberia inaelekea kupoteza zaidi ya dola za Marekani milioni 14 kwa mwaka, kutokana na hasara za kiakili za siku zijazo zinazohusiana na kutonyonyesha."


Shirika la Afya Ulimwenguni na UNICEF wanapendekeza kwamba watoto waanzishe kunyonyeshwa ndani ya saa ya kwanza baada ya kuzaliwa na kunyonyeshwa maziwa ya mama pekee kwa miezi 6 ya kwanza ya maisha.

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu